Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda amemuomba Rais John Magufuli kuwasamehe wale wanaorejesha fedha walizopewa, na Mkurugenzi wa kampuni ya VIP Engendering, James Rugemalira ambazo zimetokana na sakata la Escrow.
Shibuda ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja kuwasilisha kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) shilingi milioni 40 alizopewa na Rugemarila.
Aidha Shibudaa amesifu kitendo cha Ngeleja kurejesha fedha hizo akiwataka wengine waliopata gawio la Escrow, kuchukua uamuzi kama huo huku akiwaombea msamaha.
James Rugemalira ambaye pia alikuwa na mmiliki mwenza wa zamani wa IPTL na Mwenyekiti mtendaji wa PAP, Habi nder Seth Sigh walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka sita ikiwa ni pamoja na uhujumu uchumi.
