Shughuli ya kumuapisha Odinga kama rais wa Kenya zaahirishwa.

In Kimataifa, Siasa

Muungano mkuu wa upinzani nchini Kenya NASA, umetangaza kuahirishwa kwa shughuli ya kumuapisha kinara mkuu wa muungano huo Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama rais na makamu wa rais mtawalia wa Jamhuri ya Kenya.

Shughuli hiyo ilikuwa imepangiwa kuandaliwa Jumanne tarehe 12 mwezi huu.

Katika taarifa iliyotolewa leo na muungano wa NASA ni kuwa tarehe mpya ya kuapishwa kwa Bw. Odinga na Musyoka, na pia kuzinduliwa kwa mabunge ya wananchi itatangazwa baadaye.

Odinga alijiondoa kwenye uchaguzi mkuu ambao ulifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.

Uchaguzi huo wa tarehe 26 ulikuwa ni marudio ya uchaguzi mkuu, baada ya mahakama ya juu nchini nchini Kenya kufuta matokeo ya uchaguzi wa tarehe 8 mwezi Agosti mwaka huu.

Wakati wa kuapishwa kwake tarehe 28 mwezi uliopita, Rais Uhuru Kenyatta aliahidi kuunganisha taifa katika muhula wake wa pili uongozini katika sherehe ambayo ilisusiwa na viongozi wa upinzani.

Akihutubu baada ya kula kiapo uwanjani Kasarani, Nairobi, kiongozi huyo alisema ameyasikia baadhi ya mapendekezo ya upinzani na atazingatia baadhi.

Hata hivyo aliwahimiza viongozi wa upinzani kuheshimu sheria na katiba ya nchi hiyo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

RC MBEYA AFANYA UZINDUZI ZOEZI LA UGAWAJI VITAMBULISHO VYA (NIDA)

Mkuu wa mkoa wa mbeya Mhe. Comrede Juma Zuberi Homera amefanya uzinduzi wa wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho

Read More...

MAADHIMISHO YA WATOTO DUNIANI YAFANYIKA ARUSHA

Siku ya watoto duniani kitaifa imeazimishwa hapa jiji Arusha katika hoteli ya mount meru na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu