Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Mstaafu Emmanueli Maganga, ameagiza kusitishwa mara moja shughuli zote za Kilimo katika msitu wa Kagera nkanda.
Brigedia Maganga amesemimisha shuguli hizo, wakati uongozi wa mkoa ukikamilisha taratibu za ugawaji wa maeneo ya msitu huo, uliotolewa kwa wakulima na rais Dk John Pombe Magufuli.
Amewaagiza viongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Wilayani Kasulu, kuharakisha taratibu na kupima sehemu ya eneo la msitu huo, ili wananchi waweze kugawiwa na kuanza shughuli zao za kilimo.
Maganga ametoa maelekezo hayo Wilayani kasulu, ikiwa ni utekelezaji wa tamko la Rais Magufuli, alilolitoa wakati wa ziara yake Mkoani Kigoma mwezi Juni mwaka huu.
