siku 40 zasalia Uchaguzi Mkuu ufanyike Kenya.

Huku zikiwa zimesalia siku 40 kwa uchaguzi mkuu kufanyika, wanasiasa wako mbioni kujipigia debe na kuwarai wananchi kuwapigia kura ifikapo Agosti nane mwaka huu.

Katika karne hii ya mitando ya kijamii, wanasiasa hawa na wafuasi wao wametumia fursa hii kueneza kampeni zao kote kote.

Waziri wa usalama wa ndani wa Kenya, Joseph Nkaisery amewaonya wananchi wa Kenya wakiwemo wanasiasa dhidi ya kutumia mitandao ya kijamii kueneza chuki.

Badala yake, Nkaisery amewaomba wananchi kutumia simu zao za mkononi kuwarekodi wanasiasa wanaoneza ukabila na kuwachochea wananchi, na kusambaza video hizo pamoja na sauti ili kusaidia wanasiasa hao kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Pia amewataka wanasiasa kufanya kampeni zao kwa amani bila kueneza chuki ili uchaguzi ufanyike na umalizike  kwa wakati.

Exit mobile version