Siku ya mwisho ya maandamano mjini Istanbul kiongozi wa upinzani kuhutubia mkutano wa hadhara

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Uturuki Kemal Kilicdaroglu anatarajiwa kuhutubia mkutano wa hadhara mjini Istanbul ikiwa ni siku ya mwisho ya maandamano ya karibu mwezi mmoja, hatua ambayo iliyolenga kumpinga rais Recep Tayyip Erdogan.

Kemal wa chama kisichofungamana na dini cha Republicans People, CHP alianzisha matembezi ambayo hayajawahi kushuhudiwa ya Kilomita 450 kutoka Ankara hadi Istanbul kulalamikia kukamatwa kwa mmoja wa wabunge wake.Serikali imeyapuuza matembezi hayo ikisema ni tukio la usumbufu la kujitafutia umaarufu.

Maelfu ya watu wanatarajiwa kuhudhria maandamano hayo ambayo huenda yakawa ni makubwa kabisa ya upinzani kuwahi kushuhudiwa Istanbul tangu maandamano ya umma ya mwaka 2013 dhidi ya utawala wa Erdogan kupinga mipango ya ujenzi mpya katika bustani ya Gezi iliyopo mjini humo.

Kiongozi huyo wa CHP aliwasili kwenye viunga vya Istanbul siku ya Ijumaa na kulakiwa na maelfu waliopanga mstari barabarani bila ya kujali joto lililosababishwa na jua kali.

Exit mobile version