WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) GEORGE SIMBACHAWENE, amemwagiza mkuu wa mkoa wa Mara Dr.CHARLES MLINGWA kuingilia kati mradi wa kilimo cha miwa na kiwanda cha kutengeneza sukari ,ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati.Waziri huyo amemtaka mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Tarime mkoani Mara APOO TINDWA , kuhakikisha mradi wa shamba la miwa pamoja na kiwanda cha sukari unakamilika haraka kama ilivyokusudiwa.Waziri simbachawene ametoa kauli hiyo mjini Dodoma wakati akizungumza na Madiwani,Wenyeviti wa vijiji na wajumbe wa halmashauri ya serikali ya vijiji wa wilaya ya Tarime.
Amesema kuwa uwekezaji wa viwanda na kilimo ni agenda kubwa sana katika taifa hivyo basi mradi huo unatakiwa utekelezwe haraka.Pia ameitaka halmashauri hiyo kuhakikisha inasimamia mikataba ambayo vijiji vinaingia na mwekezaji ili kuweza kuwasaidia kutokudhurumiwa na mwekezaji.
