Kamati ya Olimpiki Tanzania TOC, imemuengua mwanariadha Alphonce Simbu katika kikosi cha timu ya Taifa cha Riadha kinachojiandaa na Michezo ya Madola huku akiwa ameanza kupiga hesabu za London Marathon 208.
Katibu Mkuu wa TOC Filbert Bayi amesema kwamba, kwenye orodha ya wanariadha wa Tanzania watakaokwenda madola Simbu hayumo.
Suala la Simbu limetokana na kukabiliwa na mashindano ya Madola na Mbio za London Marathon, ambazo zote zitafanyika Aprili mwakani huku zikipishana kwa siku chache na kiutaratibu mwanariadha wa marathoni, anapaswa kupumzika kwa miezi mitatu kati ya mbio na mbio.
