Siri ya uwanja wa Azam complex hii hapa.

Uongozi wa klabu ya Azam FC umefichua siri ya uwanja wao
wa Azam complex chamazi kuendelea kuwa bora wakati wote,
tofauti na viwanja vingine ambavyo hukosa mvuto, kila ya
msimu wa ligi unapofikia tamati.


Meneja wa uwanja wa Azam Complex Chamazi Sikitu Kilakala
amesema uwanja wao umekua na mtazamo wenye ubora siku
zote kutokana na uwepo wa wafanyakazi siku zote ambao
wanatimiza majumuku yao ya kazi, hata kama msimu wa ligi
umemalizika.


Amesema uwajibikaji wa kila mmoja uwanjani hapo umekua
chachu ya kuhakikisha kila idara inatimiza majukumu yake, kwa
kuhakikisha uwanja unakua salama wakati wote.


Sikutu amesema kutokana na umakini wanaoendelea kuufanya
uwanjani hapo, wanaamini Azam Complex Chamazi itaendelea
kuwa somo kwa klabu nyingine za soka nchini ambazo
zimedhamiria kujenga viwanja vyao binafsi.

Exit mobile version