Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP simon siro, amewaomba viongozi wa dini na wanasiasa mkoani Iringa, kushirikiana katika kutokomeza vitendo vya ulawiti na ubakaji, ambavyo vinazidi kushamiri mkoani humo.
IGP Siro ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari, katika ziara yake ya kikazi ya siku moja mkoani humo.
Amesema ili vitendo hivyo vitokomezwe ni lazima elimu izidi kutolewa kwa jamii, hususani masuala ya imani za kishirikina ambayo yametajwa kuwa chanzo kikubwa cha kuchangia matukio hayo.
Aidha IGP Sirro amewasihi askari kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya sheria, bila kumuonea mtu yoyote kwakuwa hakuna mtu ambaye yupo juu ya sheria.
