SLAA – “Migogoro ya Ardhi husababaisha shughuli za kiuchumi kukwama”

In Kitaifa

TANZANIA ikiwa leo inaadhimsha siku ya Makazi Duniani,inaelezwa kuwa bado kumekuwepo na changamoto ya migogoro ya Ardhi ambayo husababaisha baadhi ya shughuli za kiuchumi kukwama.

 Waziri wa Ardhi,Nyumba na maendeleo ya Makazi,JERRY SILAA wakati wa kilele cha Maadhimisho hayo yaliyofanyika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Kutokana na kuwepo Kwa hali hiyo,Waziri SILAA  amesema Serikali kwakuliona hilo   ipo  katika maboresho ya Sera ya Ardhi ambayo italeta suluhisho katika suala la umiliki wa Ardhi.

Amesema kumekuwepo na changamoto ya Ujenzi holela Pamoja na umiliki Wa Ardhi bila kuviendeleza jambo ambao limekuwa likwamishama ukuaji Wa uchimi na kikwazo katika Sheria kutokuwa na hatua zozote,hivyo maboresho ya Sheria yatakuwq ni suluhisho.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na maendeleo ya makazi,ANTHONY SANGA amesema kuwa Muda mwingi wamekuwa wakihangaika na migoro ya ardhi hasa ujenzi holela ambao  tayari  wameshafanya tathmini nakuona wanatakiwa waelekeze nguvu kubwa katika suala hilo pamoja na maendeleo ya ardhi na makazi.

Madhimisho ya Siku ya Makzi Duniani yanabebwa na Kaulimbiu  isemayo”Uchumi himilivu wa Miji,Miji kama kichocheo ya ukuaji na ufufuaji  wa uchumi,”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

DC Magoti apiga Marufuku pikipiki kubeba mkaa.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani ndugu PetroMagoti,amepiga marufuku piki piki kubeba mkaa katika Wilayahiyo kuanzia leo July

Read More...

Hali ilivyo Kenya sasa baada ya maandamano

Baada ya maandamano yaliyofanyika nchini Kenya juu ya Muswa wa sheria ya Fedha,leo tumezungumza na ndugu Daniel Orogo mchambuzi

Read More...

Rais wa Msumbiji kufungua maonesho ya sabasaba

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ambaye anatarajiwa kuwasili nchini kesho kuanza ziara ya kikazi, anatarajiwa kufungua rasmi Maonesho ya

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu