Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na vikosi vya
SMZ Mhe Masoud Ally Mohamed,amezindua soko la kisasa la
samaki la Msuma Fish Market maeneo ya Amani Zanzibar,
eneo ambalo ni maarifu kwa uuzwaji wa samaki.
Akizungumza katika eneo hilo amewataka wafanyabisha kuacha
kuendelea kufanya ukaidi wa kuendelea kufanya biashara hiyo
maeneo ya stand ya magari,akibainisha lengo sio kufukuzana
bali ni kuwataka wafanyabishara kwa pamoja kuwepo kwenye
soko hilo.
