Somalia imesaini mkataba wa utulivu wenye lengo la kuimarisha jeshi lake na kufufua uchumi wake uliodorora.
Baada ya kusainiwa mkataba huo kati ya Somalia na mtandao wa kimataifa, Rais Mohammed Abdullahi Mohamed amesema katika mkutano wa mjini London Uingereza kwamba siku ya kusaini mkataba huo ni ya kihistoria kwa Somalia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ambaye alikuwa miongoni mwa wenyeji wa hafla hiyo, amesema Somalia itakuwa na mafanikio.
Mkataba huo una lengo la kufanya kazi ya kuipatia msamaha wa madeni Somalia na kuisaidia kupambana na wapiganaji wa kundi la mitazamo mikali ya Kiislam al-Shabaab, ambalo kwa miaka kumi limekuwa likijaribu kuipindua serikali ya Somalia.
