Spika aeleza jinsi Lissu alivyoshambuliwa.

In Kitaifa, Siasa

Spika wa Bunge Job Ndugai amesema kuwa, mwanasheria Mkuu wa Chadema na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, alishambuliwa kwa risasi kati ya 28 hadi 32, huku tano zikimpata mwilini.

Lissu alishambuliwa jana Alhamisi kabla hajashuka kwenye gari, baada ya kumaliza kikao cha Bunge na alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kabla ya kusafirishwa saa sita usiku, kuelekea Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi Kenya.

Akitoa taarifa ya tukio hilo kwenye kikao cha Bunge leo Ijumaa, Ndugai amesema risasi mbili zilimpata Lissu kwenye miguu, mbili tumboni na moja kwenye mkono.

Pia kumekuwepo na maswali mengi na mitizamo tofauti kwa baadhi ya watu, juu ya Tundu Lissu kupelekwa Nairobi kwa matibu, hili nalo mheshimiwa spika amelifafanua.

Baada ya kutokea tukio hilo pia baadhi ya wabunge kupitia mitandao ya kijamii, wamekuwa wakiandika mambo mbali mbali juu ya tukio hilo.

Hilo nalo mheshimiwa spika amelizungumzia, pamoja na kuelezea kiasi cha fedha kilichopatika kusaidia matibabu ya Lissu baada ya wabunge kukubali kutoa nusu ya posho zao za siku moja.

Wakati huo huo Marekani imeeleza kusikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

Taarifa ya Ubalozi wa Marekani nchini iliyotolewa kupitia ukurasa wake wa Facebook imesema kuwa, Marekani inalaani kitendo hiki cha kipuuzi na cha kutumia nguvu.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu