Spika wa bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania Job Ndugai, ametoa ufafanuzi juu ya kauli ya mbunge Godbless Lema aliyoitoa akiwa jijini Nairobi.
Akiwa jijini Nairobi Godbles Lema alizungumzia maswala mbali mbali, likiwemo la spika kumuita mbunge Saidi kubenea katika kamati ya ulinzi na usalama ya bunge akisema ni sababu za mapenzi.
Pia Godbless Lema alitaka Bunge kusimama kwa muda kwa maana ya kuarishwa, baada ya tukio la mbunge Tundu lissu kupigwa risasi.
Lakini pia Spika ndugai ametolea ufafanuzi swala lililozungumzwa na Lema, kuwa serikali na bunge haijatoa mchango wowote kwenye matibabu ya Tundu lissu.
