Spika wa Bunge ajiuzulu akipinga vitendo vya Serikali.

In Kimataifa

Spika wa Bunge la Ethiopia Abadula Gemeda, amejiuzulu nafasi hiyo ikiwa ni siku mbili kabla ya kufunguliwa kwa vikao vya bunge hilo.

Kwa mujibu wa tovuti maarufu ya Addis Standard, Gemeda amechukua uamuzi huo wikendi iliyopita kama ishara ya kupinga vitendo vya Serikali ya nchi hiyo, katika masuala ya ulinzi kwenye majimbo ya Oromia na Somali.

Sababu kuu imeelezwa kuwa ni ukosoaji wa namna ambavyo Serikali inavyotumia vikosi vya ulinzi katika maeneo hayo, wakati ambapo watu 50 wameripotiwa kufa na zaidi ya watu 150,000 wamepoteza makazi kutokana na mgogoro wa rasilimali unaohusisha ukabila.

Kabla hajawa Spika wa Bunge hilo tangu mwaka 2010, Gemeda aliwahi kuwa Gavana wa jimbo la Oromia na pia Waziri wa Ulinzi.

Spika mpya wa Bunge hilo anatarajiwa kuchaguliwa mara tu wabunge watakapokutana wiki hii.

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu