Spika wa Bunge Venezuela amelitaka jeshi kuanzisha mazungumzo na kusaidia kupata suluhu ya mgogoro wa kisiasa.

In Kimataifa
   Spika wa Bunge lenye wapinzani wengi nchini Venezuela, Julio Borges amelitaka jeshi la nchi hiyo kuanzisha mazungumzo na kusaidia kupata suluhu ya mgogoro wa kisiasa.
Jeshi linamtii rais wa nchi hiyo, Nicolas Maduro ambaye amekuwa akipinga shinikizo la upinzani kuitisha uchaguzi mapema.
Borges amemtaka waziri wa ulinzi, Vladmir Padrino Lopez, kukutana na viongozi wa upinzani na kusikiliza hoja zao.
Amesema jeshi halitakiwi kuegemea upande mmoja, kazi yake ni kutetea katiba ya Venezuela, ambayo upinzani inasema inatishiwa.
Mapema mwezi huu, Rais Maduro alitangaza mipango ya kuunda bunge jipya kwa ajili ya kuandika katiba mpya

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

JUMLA YA WATU 2249 VISIWA VYA MULEBA WAPATIWA ELIMU YA UGONJWA WA MARBURG .

Baadhi ya Watalaam wa Afya kutoka Wizara ya Afya wakitoa Elimu katika kisiwa Cha Rushonga kilichopo ndani ya ziwa

Read More...

MAANDALIZI DIRA YA MAENDELEO 2050 YAANZA

SERIKALI  imeanza mchakato Wa kuandaa Dira Mpya ya Maendeleo 2050 ambapo wadau wote katika maeneo yao wametakiwa kushiriki kikamilifu

Read More...

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu