Leo ni siku ya afya ya akili duniani, ambapo maudhui ni afya njema ya akili pahala pa kazi ili kuongeza tija.
Shirika la afya ulimwenguni WHO linasema kuwa, kiwewe na msongo wa mawazo husababisha kupungua kwa tija, na hivyo kuleta hasara ya dola trilioni moja kila mwaka duniani.
Takwimu za WHO zinaonyesha kwamba, zaidi ya watu milioni 300 ulimwenguni wanakabiliwa na kiwewe na msongo wa mawazo, miongoni mwao wakiwa ni wafanyakazi.
WHO inasema afya njema ya akili pahala pa kazi, ni jambo muhimu kwa kuzingatia kuwa kipindi kikubwa cha utu uzima mtu hukitumia akiwa kazini.
Hivyo WHO imesihi mataifa kutumia siku ya leo, kuangazia na kuhamasisha umuhimu wa afya ya akili ili kuimarisha afya hiyo.
Antenna imepiga story na Daktari Iman Nkolela kutoka……na hapa anaelezea juu ya tatizo hili la afya ya akili.
