Taasisi ya kuzuia na kupambana narushwa TAKUKURU imeita Waandishi leo Dar es salaam na kutoa onyo kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari ambae alipeleka ushahidi wa tuhuma za Madiwani wa CHADEMA kupewa rushwa ili wahamie CCM Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Valentino Mlowola amesema Mh,Nassari na wenzie Ni kama wanataka kulifanya hili swala kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria,na kusema anamuonya Mh. Nassari kwa hilo,Na kumtaka aachie Takukuru kazi hiyo ya uchunguzi vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake,Kwani Takukuru haifungamani na upande wowote.
Lakini pia Mkurugenzi huyo wa Takukuru Bw.Valentino amezungumzia kuhusiana na wale wanaozungumza kwanini malalamiko hayo hayafiki mahakamani kwa haraka na kusema Takukuru in aongozwa na sheria mwenendo mashtaka ambapo ushahidi ukikamilika ndipo inaweza kwenda mahakamani.
