SHIRIKA la hifadhi za Taifa (TANAPA) limeahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa baraza la waislamu BAKWATA wilaya ya Arumeru ,kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa jengo la madrasa katika msikiti wa Mji Mwema uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.
Akizungumza na viongozi wa baraza hilo ofisini kwake katika hafla fupi ya kukabidhiwa cheti cha pongezi kwa mchango wa Tanapa kusaidia ujenzi wa jengo hilo, mkurugenzi wa shirikika hilo,Allan Kijazi amesema kwamba shirika hilo limekuwa na utaratibu wa kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo Elimu kwa lengo la kuunga mkono Sera ya Serikali .
Kijazi,amesema kwamba Tanapa linaunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano, hususani katika kusaidia na kunyanyua sekta ya elimu ,na kwa umuhimu huo kila mwaka hutenga kiasi cha sh,2.5 bilioni, kusaidia Elimu Nchini.
katika mwaka huu wa fedha 2017/18 Tanapa imetumia zaidi ya sh,2 bilioni katika miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na kujikita zaidi katika kusaidia sekta ya afya na elimu nchini.
