TANAPA kutoa milioni 10 kwa BAKWATA Arumeru.

SHIRIKA la hifadhi za Taifa (TANAPA) limeahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni 10 kwa baraza la waislamu BAKWATA wilaya ya Arumeru ,kwa ajili ya kusaidia  ujenzi wa jengo la madrasa katika msikiti wa Mji  Mwema uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha.

Akizungumza na viongozi wa baraza hilo ofisini kwake katika hafla fupi ya kukabidhiwa cheti cha pongezi kwa mchango wa Tanapa kusaidia ujenzi wa jengo hilo, mkurugenzi wa shirikika hilo,Allan Kijazi amesema kwamba shirika hilo  limekuwa na utaratibu wa kusaidia sekta mbalimbali ikiwemo Elimu kwa lengo la kuunga mkono Sera ya Serikali .

Kijazi,amesema kwamba Tanapa  linaunga mkono juhudi za serikali ya Awamu ya Tano, hususani katika kusaidia na kunyanyua sekta ya elimu ,na kwa umuhimu huo  kila mwaka hutenga kiasi cha sh,2.5  bilioni, kusaidia Elimu  Nchini.

 katika mwaka huu wa fedha 2017/18 Tanapa imetumia zaidi ya sh,2 bilioni katika miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwa ni pamoja na  kujikita zaidi katika kusaidia sekta ya afya na elimu nchini.

 

Exit mobile version