Tanzania Nchi ya kwanza kuendesha Treni kwa umeme Afrika Mashariki- Dkt. Kalemani

Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani amesema Tanzania ni ya kwanza Afrika Mashariki kuendesha treni ya umeme.

Dkt. Kalemani ameyasema hayo eneo la Kingolwira Mkoani Morogoro wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa Mradi maalumu wa Kusafirisha umeme utakaotumika katika reli ya kisasa ya (SGR).

Dkt. Kalemani aliongeza kuwa, katika kutekeleza miradi ya huduma wezeshi za mradi wa SGR, tayari Wizara ya Nishati kupitia TANESCO wako katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi mahususi wa kusafirisha umeme kwa ajili ya kendesha treni hiyo.

Aidha, awamu ya kwanza ya utekelezaji kutoka Dar es salaam hadi Morogoro, yenye urefu wa kilomita 161 ambao umekamilika kwa asilimia 94.

Exit mobile version