TANZIA: WAZIRI MSTAAFU WA KILIMO AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo Mhe. Herman Kirigini Amefariki Dunia.

Akithibitisha Kifo hicho Mtoto wa Marehemu Paul Kirigini amesema


“Kwa masikitiko makubwa sana, naomba kutoa taarifa zenye majonzi makubwa ya kifo cha Mhe Herman Kirigini (Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini) aliyetutoka jioni ya jana jioni tarehe 23 mei -2023.

Marehemu Herman Kirigini alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini (1980-1985), Waziri wa Kilimo na Mifugo, n.k. Marehemu ni mzaliwa na Kijiji cha Muryaza, Wilaya ya Butiama.”

Taarifa zaidi zitaendelea kutatolewa na familia ya marehemu

Exit mobile version