Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza sherehe za wakulima Nane Nane Kanda ya Kaskazini, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo ametoa tamko la TASSO kutoshugulika na maandalizi na Usimamizi wa sherehe hizo kama miaka mingine iliyopita kutokana na Usimamizi Usioridhisha kwa Wakulima
Akizungumza na Wakuu wa Wilaya, na Wakurugenzi wa Kanda ya Kaskazini katika kikao cha pili cha Maandalizi ya Sikukuu ya Wakulima,Gambo amesema sababu ya serikali kuwaondoa TASSO ni kutokana na usimamizi hafifu ambao umekuwa ukifanywa na TASSO kwa nchi nzima.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Manyara John Bendera amesema kanda ya kaskazini imepokea agizo la serikali bila vipingamizi hivyo watahakikisha shughuli hizo zinafanyika kwa ufanisi mkubwa.
Nae mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Mh. Anna Mgwira amesema ili kuweza kukamilisha zoezi hilo ,panatakiwa kuwa na ulinzi na usalama wa kutosha ,ambapo amewataka wakulima wajiandae ikiwa ni pamoja na kubadilisha bidhaa zao kutoka malighafi kuingia viwandani.
