Tatizo la nguvu za kiume zatinga bunge.

 

Sakata la upungufu wa nguvu za kiume ambalo limekuwa changamoto kubwa kwa baadhi ya wanaume nchini, limeibua sintofahamu bungeni leo.

 

Hali hiyo imeibuka baada ya mbunge wa Konde Khatibu Saidi Haji kupitia CUF, kutaka kujua serikali imejipanga vipi katika kukabiliana na tatizo hilo.

Akijibu swali hilo Naibu waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Daktari Hamisi Kigwangala, amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kusema kuwa, serikali haina jibu la moja kwa moja kuweza kuwapa wananchi, kwani tendo la ndoa hufanyika faragha baina ya wanandoa.

Dkt Kigwangala ameeleza pamoja na usiri uliopo kuhusu tatizo hilo, lakini kuna vitu wanaweza kufanya ili kukabiliana nalo, ambapo huwenda likasaidia kuokoa ndoa na kuweza kuwapatia wanandoa watoto.

Baada ya Dr Kigwangala kutoa maelezo hayo,kwa upande wake  waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu, amesema serikali imepiga marufuku waganga wa tiba za asili nchini na wadau mbalimbali, ambao wanauza dawa zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume kinyume na sheria.

Exit mobile version