Watanzania wametakiwa kuwa na utamaduni wa kufuata sheria na kanuni za mitandao ili kuweza kuepukana na changamoto ya ukosefu wa mawasiliano hapa nchini
Hayo yamelezwa na Mwandisi wa Idara ya Leseni kutoka mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Kadaya Baluhya, wakati akitoa semina ya watoa huduma za mawasiliano na wamiliki wa vyombo vya habari uliofanyika mkoani Arusha
Amesema lengo la semina hiyo ni kuwawezesha wadau wa vyombo vya habari na mawasiliano nchini, kujua sheria za kulinda mawasiliano kwani hii itasaidia kupunguza tatizo wa uhalifu kwa baadhi ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii
Akizungumzia sheria ya makosa ya mitandao Kadaya amesema kuna baadhi ya watu wanatumia picha za Ajali kwa kutuma kwenye mitandao bila kujali utu hivyo sheria itachukua mkondo kulivalia njuga swala hilo
Halikadhalika amewataka wananchi kuwa makini katiaka maswala ya mawasiliano na kuweza kushirikiana na mamlaka hiyo ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi
