Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na Tembo asubuhi ya leo August 3 2022.
Yonael na Wenzake wa (3) ambao ni Dhihiri Rajabu, Jonson Mtwatui na Peter Jacob walikuwa wakielekea Ziwa Jipe kwa ajili ya Shughuli zao za kila siku za Uvuvi ambapo walivamiwa na Tembo hao na Tembo Kumuua huku wenzake wakibahati kuokoka kwa Kukimbia na Kupanda kwenye Miti.
Hata hivyo Matukio ya watu kuuwawa yamekithiri katika Vijiji hivyo Jirani vya Kigonigoni, Kwakoa, Ngulu, Butu, Ruru na Toloha ambapo Mpaka sasa zaidi ya Watu 10 wamepoteza maisha kwa Matukio ya Tembo hao ambao Wamezagaa kila Mahali huku Wananchi wakilalamikia Serikali kutochukua Hatua.
Jeshi la Polisi pamoja na Tanapa wamefika eneo hilo na Kuuchukua mwili wa Marehemu kwa ajili ya Uchunguzi zaidi ambapo baada ya kufika kumetokea Vurugu kati ya Wananchi na Polisi kwa kile wananchi walichosema Wamechoka Matukio haya Kujirudia ambapo baadae Polisi waliwatuliza wananchi na kusema Watachukua hatua.
Ukiachana na Matukio ya Kuuwawa Watu, Tembo hao wamewatia Wananchi Umaskini katika Vijiji hivyo ambapo wamekuwa wakiharibu Mazao kila Msimu kitu Kinachofanya Wananchi hawana Chakula.
Tunaendelea Kumtafuta RPC wa Kilimanjaro, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga na Mbunge wa Mwanga
Imeandikwa na Hamis A. Hamis
Radio5Updates @radio5tz
