Teresita za Soka Ulaya

In Kimataifa, Michezo

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 37, anapanga mazungumzo na wakala wake kuhusu mustakabali wake wa Manchester United baada ya kukatishwa tamaa na maisha huko Old Trafford. (Star)

Kiungo wa kati wa Uingereza Declan Rice, ambaye analengwa na Chelsea na Manchester United na City, amesisitiza nia yake ya kushinda mataji na kucheza Ligi ya Mabingwa, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 aliwatuliza mashabiki wa West Ham kwa kuelezea uvumi juu ya hatma yake kama “kelele tu”. (Standard)

Paul Pogba atalazimika kulipa posho kwa kandarasi kubwa ya mwisho ya maisha ya kiungo huyo wa kati wa Manchester United na Ufaransa mwenye umri wa miaka 28 ikiwa anataka kukamilisha ndoto yake ya uhamisho wa bure msimu huu wa joto. (Mirror)

Mlinda mlango wa Chelsea mwenye thamani ya pauni milioni 72 Kepa Arrizabalaga, 27, anaweza kuondoka Stamford Bridge msimu huu wa joto huku The Blues wakiwa hawajapanga kumzuia mchezaji huyo wa Uhispania ikiwa anataka kuondoka. (Sun)

Barcelona wanashinda mbio za kumsajili kiungo wa kati wa AC Milan na Ivory Coast Franck Kessie msimu huu wa joto. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 pia analengwa na Liverpool. (Marca)

Mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane, 29, yuko tayari kuondoka katika klabu hiyo ya Anfield huku Barcelona na Real Madrid wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal. (Goal, via Mirror)

Leicester City wamepunguza dau la kumnasa Youri Tielemans, 24, kutoka pauni milioni 60 hadi pauni milioni 35, huku Arsenal na Manchester United wakiwa katika mbio za kumnunua kiungo huyo wa kati wa Ubelgiji msimu huu. (Het Nieuwsblad,viaMetro)

Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta amekiri kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu huu kunaweza kuwa muhimu katika kumfunga winga wa Uingereza Bukayo Saka, 20 – ambaye anahusishwa na Liverpool – kwa kandarasi mpya. (Express)

Mlengwa wa Manchester United Manuel Akanji anataka kuongeza mishahara yake maradufu huku Borussia Dortmund wakiweka bei wanayohitaji kumnunua mlinzi huyo wa Uswizi, 26. (Bild, via The Sun)

Mkufunzi wa Uhispania Luis Enrique, 51, ameibuka kuwa mgombea wa kushtukiza kwenye kibarua cha kocha wa Manchester United. (Star)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu