TETESI ZA SOKA LEO NOVEMBA 11, 2022

In Kimataifa

Borussia Dortmund wana imani kuwa wanaweza kumbakisha kiungo wa kati wa England Jude Bellingham mwenye umri wa miaka 19 hadi mwisho wa msimu huu, licha ya vilabu kadhaa kuu vikiwemo Chelsea, Liverpool, Manchester City na Manchester United kuwindwa na klabu hiyo. (90Min)

Paris St-Germain wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid Joao Felix na mabingwa hao wa Ufaransa wanaweza kujaribu kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 23 kwa mkopo wakati wa dirisha la Januari. (Le Parisien, via Marca)

Roma wataelekeza mawazo yao kwa beki wa kulia wa Barcelona Mhispania Hector Bellerin, 27, wakati huu ambao Diogo Dalot wa Ureno, 23, waliokuwa wanamfuatilia akionekana sehemu muhimu ya mipango ya Manchester United. (Calciomercato)

Gossip
Maelezo ya picha,Bellerin

Senegal itatumia waganga katika jaribio la kumsaidia mshambuliaji wa Bayern Munich Sadio Mane, 30, apone jeraha kwa wakati ili acheze Kombe la Dunia. (Mail)

Beki wa Canada Alphonso Davies anaamini atakuwa fiti kwa Kombe la Dunia baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kupata majeraha ya msuli wa paja wakati akiichezea Bayern Munich dhidi ya Hertha Belin Jumamosi iliyopita. (Mail)

Mshambulizi wa Everton na England Dominic Calvert-Lewin, 25, ataonana na mtaalamu ili kujua ukubwa wa tatizo lake la bega lililoteguka. (Guardian)

Gossip
Maelezo ya picha,Mane akitibiwa majeraha uwanjani

Aston Villa inasaka mshambuliaji mkubwa katika dirisha la uhamisho la Januari, wakati mlinzi wa Villarreal Mhispania Pau Torres, 25, pia anavutiwa na meneja aliyeteuliwa hivi karibuni Unai Emery. (Football Insider)

Tottenham itaweka kipaumbele kwa beki wa kulia anayecheza kama winga na mshambuliaji wa akiba katika dirisha la usajili la Januari. (90Min)

Barcelona wanaweza kumruhusu mshambuliaji wake Mholanzi Memphis Depay, 28, kuondoka katika dirisha la usajili la Januari. (Caughtoffside)

Gossip
Maelezo ya picha,Depay

Southampton itailipa klabu ya Ligi Daraja la Kwanza, Luton Town zaidi ya pauni milioni 4 kama fidia kwa ajili ya meneja Nathan Jones, ambaye alitangazwa kuchukua nafasi ya Ralph Hasenhuttl aliyetimuliwa Saints Alhamisi. (Telegraph)

Mlinzi wa zamani Gerard Pique anasema atawania urais wa Barcelona akiangazia shughuli zake nyingine za kibiashara baada ya kustaafu soka wiki hii. (ESPN)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu