Tetesi za Soka Ulaya

Arsenal wana nia ya kumsajili nyota wa Barcelona Alejandro Balde huku beki huyo wa pembeni wa Hispania mwenye umri wa miaka 19 akiwa bado hajasaini mkataba mpya na klabu yake. (Sport)

Newcastle wanajiandaa kumnunua mshambuliaji wa Bayer Leverkusen Moussa Diaby mwenye umri wa miaka 23 huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 23 akihusishwa kwa muda mrefu kutaka kuhamia ligi kuu England, (Bild)

Aston Villa wanaaminika kukaribia kufanikiwa katika mazungumzo ya kumsajili mlinzi wa Hispania Alex Moreno kutoka Real Betis, 29. (Football Insider)

Maelezo ya picha,Moreno

Atletico Madrid wanataka kumsajili tena kinda aliyewahi kuchecheza timu zao za vijana mhitimu zamani wa anayechezea Manchester United Alejandro Garnacho lakini klabu hiyo ya Old Trafford huenda ikagoma kumruhusu Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 18 kuondoka. (Fichajes)

Manchester United wanataka kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Bosnia Edin Dzeko, 36, ambaye alikuwa na mafanikio makubwa awali akiwa na Manchester City. (Mail)

Maelezo ya picha,Dzeko

Southampton wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Celtic raia wa Japan Daizen Maeda, 25. (Sky Sports).

Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim anasisitiza kuwa klabu hiyo haihofii Tottenham kutaka kumnunua beki wa hispania Pedro Porro, 23 na kiungo wa zamani wa Spurs Muingereza Marcus Edwards, 23. (Standard).

Wakati huo huo, Tottenham wanamfuatilia kipa wa Brentford Mhispania David Raya, 27, wakitafuta mrithi wa muda mrefu wa Hugo Lloris wa Ufaransa, 36 msimu wa joto. (Telegraph)

Exit mobile version