TETESI ZA SOKA ULAYA

In Kimataifa, Michezo

Manchester United wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uingereza Tammy Abraham, 25, anapiga soka ya kulipwa katika klabu ya Roma ya Italia. (Caught offside via Manchester Evening News)

Chelsea wako tayari kujiunga na kinyang’anyiro cha kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uingereza anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni 100m Jude Bellingham, 19, kutoka Borussia Dortmund licha ya kutumia zaidi ya pauni 600m katika madirisha mawili yaliyopita ya uhamisho. (Telegraph – usajili unahitajika)

Leicester wameongeza kasi ya mazungumzo ya kandarasi na kiungo James Maddison, 26, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza akikaribia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake wa sasa. (Telegraph – usajili unahitajika)

Fati

Mshambulizi wa Uhispania Ansu Fati, 20, hana nia ya kuondoka Barcelona, ​​licha ya ofa kutoka kwa Tottenham, Arsenal na Bayern Munich, pamoja na Manchester United kumtaka. (Mundo Deportivo)

Tottenham wanafuatilia uhamisho wa mlinda mlango wa Sevilla mwenye umri wa miaka 31 kutoka Morocco Yassine Bounou, anayejulikana kama Bono, huku wakitafuta mbadala wa muda mrefu wa Mfaransa Hugo Lloris, 36. (AS – kwa Kihispania)

Aston Villa wanatarajia ofa kwa ajili ya mlinda mlango wa Argentina aliyeshinda Kombe la Dunia Emiliano Martinez, 30, msimu huu wa joto, lakini hawana shinikizo la kumuuza kwani kandarasi yake inaendelea hadi 2027. (Mail).

Yassin

Amiri wa Qatar, Sheikh Tamim bin Hamad al-Thani, anatarajiwa kutoa ofa ya zaidi ya £4bn kwa Manchester United kufikia tarehe ya mwisho ya Ijumaa. (Guardian)

Athletico Paranaense wamekataa ofa kutoka kwa Barcelona na vilabu vingine viwili kwa ajili ya mshambuliaji wa Brazil Vitor Roque, 17, ambaye pia anaripotiwa kuwindwa na Arsenal. (Bao kupitia Globo Esporte)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu