Tetesi za soka Ulaya.


Chelsea wamemuweka mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa
Leicester Ben Chilwell, 23, katika mpango wao wa uhamisho
lakini inaweza kuwagharimu mpaka kiasi cha pauni milioni 85
kumnasa mchezaji huyo. (Athletic)
Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane amezungumza na
wakala wa kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba,

27, akisema kuwa bado angependelea kumsajili mchezaji huyo.
(Le 10 Sport-in French)
Manchester United wamebainisha kuwa winga wa Velez
Sarsfield Thiago Almada,19, anawezekana akawa sehemu ya
mpango wao wa uhamisho mbadala wa winga wa Borussia
Dortmund Jadon Sancho, 20. (Manchester Evening News)
Inter Milan watamsajili mshambuliaji wa Arsenal Alexandre
Lacazette,29, endapo mshambuliaji wa Argentina Lautaro
Martinez,22, atajiunga na Barcelona. (Mundo Deportivo)
Barcelona ina mpango wa kumsaini tena beki wa kati wa
Kihispania Eric Garcia,19, kutoka Manchester City. (ESPN)

Exit mobile version