Barcelona wameanzisha mazungumzo juu ya mkataba mpya wa
mwaka mmoja kwa ajili ya Muargentina Lionel Messi,
anayetimiza umri wa miaka 33 Jumatano wiki hii. (Marca)
Chelsea wanaweza kuelekeza nia zao kwa kiungo wa safu ya
nyuma kushoto ya wa Paris St-Germain Layvin Kurzawa, 27,
iwapo hawataweza kusaini mkataba na mchezaji wa Kimataifa
wa England kutoka Leister Ben Chilell,23. (Express)
