Inter Milan wanafikiria kumnunua kiungo wa kati, Mfaransa
N’Golo Kante huku Blues wakiwa tayari kusikiliza ofa kwa ajili
ya kumuuza mchezaji huyo wa Ufaransa, 29. (Gazzetta dello
Sport, via Metro)
Zenit St Petersburg wameeleza nia yao ya kumsajili beki
anayekipiga katika klabu ya Liverpool Dejan Lovren, 31.
(Liverpool Echo)
AC Milan wanafiukiria kumnunua mashambuliaji wa Real
Madrid raia wa Serbia Luca Jovic, 22, ambaye anatekodolewa
macho na Leicester City na Arsenal. (Calciomercato,via
Leicester Mercury)
Bayern Munich wana mpango wa kuwanasa viungo wawili
wanaocheza ligi kuu ya Ufaransa, Tonguy Ndombele wa
Tottenham, 23, na Tiemoue Bakayoko. (Le 10Sport)