Tetesi za soka Ulaya.


Arsenal ina matumaini ya kukamilisha makubaliano ya pauni
milioni 22 kwa mlinzi wa Lille Gabriel Magalhaes. Everton na
Napoli pia nazo zinamnyatia mchezaji huyo wa Brazil, 22.
(ESPN)
Chelsea itakamilisha makubaliano ya mchezaji wa Bayer
Leverkusen Kai Havertz, 21, ndani ya siku 10 zijazo. Raia huyo

wa Ujerumani anataka kuhakikishiwa makubaliano ya miaka
mitano huko Stamford Bridge. (Bild, via Express)
Juventus huenda ikamtumia mshambuliaji Paulo Dybala, 26,
kama sehemu ya makubaliano ya mabadilishano na Manchester
United kumrejesha Paul Pogba katika Ligi ya Serie A. Raia wa
Argentina Dybala amesalia na miaka miwili huko.
Chelsea itafanya mazungumzo na kiungo wa kati Conor
Gallagher huku Newcastle na Crystal Palace zote zikionesha nia
ya kumsajili msimu uliopita .

Exit mobile version