Tetesi za soka Ulaya Jumatano leo Aprili 27, 2022

In Kimataifa, Michezo

Paris St-Germain wanamatumaini kwamba mshambuliaji wake mfaransa Kylian Mbappe, ambaye amekuwa akihusishwa na Real Madrid, atasaini mkataba mpya kufuatia mazungumzo yao na mama wa nyota huyo mwenye miaka 23 wiki iliyopita. (Telegraph – subscription required)

Liverpool imefanya mawasiliano na kiungo wa Ufaransa na Monaco Aurelien Tchouameni, 22. (Foot Mercato – in French)

Manchester United inapanga kuzungumza na kipa mhispania David de Gea, 31 kuhusu mkataba mpya. (90 Min)

Manchester United huenda ikaangukia pia kwa nyota wa kimataifa wa Ivory Coast Sebastien Haller, 27. Mshambuliaji huyo kwa sasa anacheza chini ya kocha ajaye wa United Erik ten Hag pale Ajax. (Sun)

Kiungo mholanzi Donny van de Beek, 25, atapewa nafasi Manchester United msimu ujao na kocha Ten Hag. (Telegraph – subscription required)

Arsenal watahitaji kutoa kitita cha £67.7m kumsajili mshambuliaji wa England Tammy Abraham, 24, kutoka Roma. (Football London)

Mlinzi mfaransa Jules Kounde anataka kuondoka Sevilla msimu wa kiangazi na nyota huyo mwenye miaka 23 anaitazama zaidi Chelsea. (Times – subscription required)

Chelsea inamfuatilia mlinzi wa Ujerumani Amos Pieper, 24, ambaye mkataba wake na klabu ya Bundesliga Arminia Bielefeld unamalizika mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Newcastle inamtaka kiungo wa Tottenham na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 26. (Express)

Kikosi hicho cha Eddie Howe’ pia kinamshawishi nyota wa kimataifa wa Reims na timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka-20 Hugo Ekitike, 19. (90min)

The Magpies pia wanamtaka mlinzi mfaransa Evan Ndicka, 22,anayekipiga na klabu ya Eintracht Frankfurt. (Bild – in German, subscription required)

Kiungo wa Wolves na Ureno Ruben Neves, 25, ana shauku ya kujiunga na Barcelona. (Sport – in Spanish)

Kuna matumaini makubwa pale Barcelona kwamba mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski, 33, anaweza kujiunga nao msimu huu akitokea Bayern Munich. (Sport – in Spanish)

Nyota wa kimataifa wa Croatia Luka Modric, 36, anajiandaa kusaini mkataba mwingine mpya Real Madrid, utakaomalizika mwaka 2023. (Fabrizio Romano)

Leeds United watajielekeza kumsajili mshambuliaji wa Wales Brennan Johnson kama watasalia ligi kuu England, na endapo pia klabu Nottingham Forest anayochezea kinda huyo mwenye miaka 20 itashindwa kupanda ligi kuu. (Mail)

Newcastle United inakaribia kumalizana na mlinzi wake raia wa Switzerland Fabian Schar, 30 kwa kumpa mkataba mpya, mkataba wake wa sasa unamalizika mwishoni mwa msimu. (Mail)

Mlinzi wa pembeni muingereza Ashley Young ataongeza mkataba wake wa kusalia Aston Villa kwa mwaka mmoja zaidi, alijiunga na klabu hiyo ya Midlands akitokea Inter Milan msimu uliopita. (Times – subscription required)

Villa iko kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo Msoctland wa Hearts Ewan Simpson. (Mail)

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

TEMBO WAUA TENA KIGONIGONI

Aliyekuwa mwananchi wa Kijiji cha Kigonigoni Wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, Yonael Kaindu Maarufu kama Mzembi, ameshambuliwa na Kuuawa na

Read More...

Waziri wa zamani wa Msumbiji ahukumiwa kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi.

Msumbiji Alhamisi imemuhukumu waziri wa zamani kifungo cha miaka 16 jela kwa makosa ya ufisadi, ikiwa ni hukumu kali

Read More...

YANGA yasaini Mkataba mpya wa Udhamini na Sportpesa

KLABU ya Yanga SC, imesaini mkataba mpya wa Udhamini Mkuu na Kampuni ya kubashiri ya Sportpesa Tanzania, wenye thamani

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu