TETESI ZA SOKA ULAYA LEO JUMANNE NOVEMBA 7, 2023

Manchester United na Newcastle United zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Rayan Cherki, 20, ambaye mkataba wake unamalizika Juni 2025. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Manchester United na Ureno Bruno Fernandes, 29, anatarajiwa kulengwa na klabu za Saudi Pro League mwezi Januari (Rudy Galetti)

Meneja wa West Ham David Moyes hayuko katika hatari ya kutimuliwa licha ya timu yake kushinda mchezo mmoja tu kati ya saba zilizopita za Premier League, lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 60 huenda asiongezwe mkataba wake ambao unamalizika msimu ujao wa joto.(Talksport)

Juventus wana imani kwamba watakubaliana kuhusu mkataba mpya wa muda mrefu na kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 28, ambaye alisaini nyongeza ya mwaka mmoja wakati wa kiangazi (90 Min)

Manchester City wana nia ya muda mrefu ya kumnunua kiungo wa kati wa Ujerumani Florian Wirtz na walimtazama mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 wakati timu yake ya Bayer Leverkusen ikiichapa Hoffenheim siku ya Jumamosi (90 Min)

Juventus na Everton zote zinamfuatilia mshambuliaji wa Borussia Monchengladbach mwenye umri wa miaka 17 Winsley Boteli. (Fabrizio Romano)

Beki wa Liverpool Ibrahima Konate, 24, alikiri kwamba amekuwa na ndoto ya kuichezea Paris St-Germain lakini kuhamia kwa mabingwa hao wa Ligue 1 si mojawapo ya “lengo” la sasa la kiungo huyo wa kati wa Ufaransa. (Canal Plus, kupitia Goal)

Mkufunzi wa Al-Ettifaq, Steven Gerrard anasema “atazunguka Ulaya” kwa ajili ya kulenga wachezaji zaidi wakati wa uhamisho huku akipania kuimarisha kikosi chake mwezi Januari. (Mail)

Kocha wa zamani wa Chelsea Frank Lampard anasema bodi ya klabu hiyo ilimnyima nafasi ya kumsajili kiungo wa kati wa Uingereza na Real Madrid Jude Bellingham, 20, alipokuwa Birmingham City .. (Obi One podcast, kupitia Talksport)

Kocha wa Oxford United Liam Manning anakaribia kuwa meneja mpya wa Bristol City(Sky Sports)

Exit mobile version