Katika kuendelea kukuza utalii wa utamaduni hapa nchini kampuni ya Tigo kanda ya kaskazini imeendeleaa kuwaunga mkono wadau wa utalii na wajasitiamali wadogo
Kampuni hiyo pia imeshiriki katika maonyesho ya siku 3 ya Masai Festival ambayo yanaendelea katika viwanja vya Ngarinaro vilivyopo jinini Arusha lengo ni kuweza kuendelea kutoa elimu mbalimbali za tigo na kuwafikia wajasiriamali kwa karibu
Hata Hivyo huduma wanazozitoa ni pamoja na Tigo Business, Mjasiriamali Boss, ambapo wameweka huduma hizo ili kila mwananchi aweze kupata huduma na kutimiza malengo yake
Akizungumza Na vyombo vya Habari Daniel Menoya Meneja wa Kanda mawasiliano ya Tigo amesema mtandao wa tigo itaendelea kushirikiana na jamii hasa katika kuufuta umaskini.
Kwa, upande wake Woinde Shisael Meneja Mawasiliano – Tigo Amesema kuwa kwa sasa Kampuni ya Tigo imefikia Asilimia 90 ℅ ya huduma, hiyo hapa nchini na pia imetoa shilingi Trilion 1 kutanua mtandao huo hapa nchini kwa kuwa wameshatanga 5G kwa kampuni hiyo Hata hivyo wamewataka wananchi kwenda viwanja vya Ngarinaro ili kuweza kujifunza masuala mbalimbali ya ujasiriamali, mitandao, na fedha ili kuweza kuepukana na changamoto mbalimbali
