TLP kuzunguka nchi nzima kuzungumzia miradi iliyotekelezwa na Serikali

In Kitaifa

Chama cha Tanzania Labour Party TLP kimeunda timu ya kuzunguka nchi nzima kuzungumzia miradi iliyotekelezwa na Serikali ya awamu tano chini ya Dkt.John Magufuli kama kuonyesha Juhudi za kuungamkono kwa vitendo kauli ya mkutano mkuu wa chama hicho.

Aidha chama hicho kimeendelea kuwapongeza Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Dkt.Agustine Mrema kwa kuchaguliwa tena kuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Makamu wake bara Bi Dominata Rwechungura na visiwani Husein Juma sanjari na kuhamasisha kukijenga chama na kuhakikisha Mh.Dkt.Magufuli anashinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao.

Akiongea na vyombo vya habari mkoani Arusha Katibu Mwenezi wa taifa wa chama hicho Geofrey Stephen amesema kuwa baada ya kamati kuu kumpitisha kwa kauli moja mgombea wa CCM Dkt. Magufuli kuwa ndie anafaa kugombea kwa mwaka huu katika uchaguzi mkuu na chama hicho kumuunga mkono mgombea huyo.

Alisema kuwa kupitia kikosi kazi hicho watapita nchi nzima kuelezea na kumnadi mgombea huyo kwa wananchi ili wafahamu utekelezaji wa serikali yake katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli ndio maana kwa kauli moja kamati kuu ikaona anafaa kuungwa mkono na chama hicho kwa nafasi ya urais.

Kwa mujibu wa Katibu huyo wa chama hicho ameeleza kuwa chama hicho kimejipanga upya ikiwa ni pamoja na kusimamisha wagombea nchi nzima kwa nafasi ya Ubunge na udiwani kwa kuwa ikumbukwe kuwa TLP ndio chuo cha wagombea.

“Kama unavyojua chama chetu kimezaliwa upya baada ya kufanya uchaguzi wa viongozi na Mwenyekiti wetu kuendelea kuwa Agustine Mrema hivyo sura mpya ya uongozi wa.chama chetu unaakisi mageuzi makubwa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu”

Awali akiongea kwenye Kikao hicho na waandishi wa habari Katibu mkuu wa chama hicho mkoa wa Arusha Kinanzaro Geofrey alieleza kuwa chama hicho mkoa wa Arusha litasimamisha wagombea kwenye majimbo yote sanjari na nafasi za Udiwani.

Alisema kuwa mfano mzuri chama hicho kwa jimbo la Arusha mjini pia kitasimamisha mgombea kwani historia inaonyesha wagombea wote waliotoka TLP ni bora hata huyu mbunge ni zao la chama chetu.

Alisema wapo wanachama wa.vyama.vyengine wanaofanya vizuri wote wametoka ndani ya chama hicho hivyo ndio maana wanajipanga kuona wananzalisha wanasiasa ambao watasaidia nchi kufikia malengo yenye tija kwa nchi yetu.

“Niwatoe hofu maamuzi ya kumpitisha mgombea wa nafasi ya Urais wa chama chetu kuwa ni Dkt.John Magufuli wa CCM yamefanywa na kupewa baraka na mkutano mkuu wa chama chetu na sio maamuzi yake pekee mwenyekiti bali ya wajumbe wote wa mkutano huo”

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

MAJALIWA ATOA RAI KWA WAMILIKI WA MALORI KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa malori nchini wawajali madereva na wahudumu wa magari hayo ikiwa ni pamoja

Read More...

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu