(TLS) kumburuza Mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam, PAUL MAKONDA.

In Kitaifa

BARAZA la Uongozi la Chama cha wanasheria nchini Tanganyika law Society (TLS) ,linatarajia kumwandikia barua Mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP kumshinikiza atoe ridhaa ili wampeleke Mahakamani Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam,PAUL MAKONDA kwa tuhuma za makosa mbalimbali  ya jinai ikiwemo kutumia vyeti feki,ujambazi wa kutumia silaha na matumizi mabaya ya madaraka.

Pia Baraza hilo limesema kuwa endapo Mkurugenzi wa mashitaka nchini DPP atakataa kutoa ridhaa yake,TLS itamfungulia mashitaka ya rejea ya kimahakama katika mahakama kuu ya Tanzania ili alazimishwe kutoa ridhaa hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Baraza hilo ambae pia ni Rais wa Chama cha wanasheria nchini TLS,Mh.TUNDU LISSU, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.

Pia amebainisha kuwa  baraza la uongozi la chama hicho limefikia maamuzi hayo baada ya kikao chake cha siku mbili na kuazimia kuchukua hatua hizo kwa lengo la kulinda utawala wa Sheria na uwajibikaji katika nchi.

Pia Baraza hilo limebainisha kuwa PAUL MAKONDA hajafanya kosa hilo tu bali kwa kitendo chake cha kuvamia ,kituo cha kurushia matangazo cha Clouds Media Group kipindi cha miezi miwili iliyopita  na kwamba amefanya makosa mengine mengi yapatayo 10 ambapo hapa anabainisha baadhi ya makosa hayo

Katika hatua nyingine pia baraza hilo limeazimia kuchukua hatua  kwakushirikiana na wadau wengine za kuhoji masuala mbalimbali ambayo yameathiri ustawi  wa jamii ya Tanzania hususan masuala ya mafao na haki za wafanyakazi.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

CCM waongeza nafasi za Wajumbe Halmashauri kuu

Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk Samia Suluhu amesema ili kupanua wigo, halmashauri kuu

Read More...

Washukiwa 25 wanaodaiwa kupanga njama za mapinduzi wakamatwa Ujerumani

Maelfu ya polisi leo wamefanya msururu wa misako kote Ujerumani wa washukiwa wa siasa kali za mrengo wa kulia

Read More...

Mkuu mpya wa chuo cha Arusha asimikwa.

Chuo kikuu cha Arusha kimemsimika mkuu mpya wa chuohicho wakati wa mahafali ya 16 ambayo yamefanyika chuonihapo.  Mkuu aliyeachia nafasi

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu