Mamlaka ya hali ya hewa Nchini kupitia kwa mkurugenzi Mkuu wake Dk Agnes Kijazi, amekutana na wanahabari kutoa taarifa kuhusu mweleko wa mvua za vuli.
Dk kijazi amesema mvua za vuli mwaka 2017 zinatarajiwa kuanza mwezi September katika maeneo mengi ya ziwa viktoria, na mwezi october 2017 katika ukanda wa Pwani.
Ameongeza kwa kusema baadaye kwenye mwezi November katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki.
Aidha Dk Kijazi amesema ongezeko la mvua linatarajiwa katika miezi ya November na December 2017, pia vipindi virefu vya ukavu vinatarajiwa kujitokeza zaidi katika mwezi october 2017.
