Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA mkoani Manyara, imetangaza nia ya kukusanya kodi kutoka kwa wafugaji na wakulima,wanaopata mapato kuanzia shilingi milioni nne kwa mwaka.
Hayo yamesemwa na Meneja wa TRA mkoani humo Joseph Mtandika, akibainisha kuwa kutokana na taratibu za kisheria, mauzo ya mifugo na mazao yao wanatakiwa kulipa kodi.
Amesema wapo wakulima na wafugaji ambao hupata mapato mengi kutokana na mauzo ya bidhaa zao lakini hujificha kulipa kodi.
Hata hivyo amesema changamoto waliyonayo ni juu ya kuwabaini watu wanaotakiwa kulipia kodi wenye sifa za namna hiyo.
