(TRA) yatangaza makusanyo ya kodi.

In Kitaifa

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetangaza makusanyo ya kodi kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa yalikuwa Sh trilioni 14.4.

Makusanyo hayo yana ongezeko la asilimia 7.67 ya makusanyo yaliyofanywa na TRA katika mwaka wa fedha wa 2015/16 ambayo yalikuwa Sh trilioni 13.3.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Walipa Kodi, Richard Kayombo amesema kwa Juni ilikusanya kiasi cha Sh trilioni 1.37.

Kayombo pia amesema mamlaka imeendelea kukusanya kodi mbalimbali ikiwemo kodi ya majengo na mwitikio wake umekuwa ni wa kiwango cha kuridhisha.

Amesema aliwashukuru wananchi wanaojitokeza katika ofisi mbalimbali za mamlaka nchi nzima ili kulipia kodi hiyo ya majengo ambayo mwisho wake wa kulipa ni Julai 15, mwaka huu.

Ameongeza kuwa TRA inatoa mwito kwa wafanyabiashara wote kutoa risiti za kielektroniki (EFDs) pindi wanapouza bidhaa au huduma na wananchi wote, kuhakikisha wanadai risiti pindi wanaponunua bidhaa au huduma

 

 

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

MAJALIWA ATOA RAI KWA WAMILIKI WA MALORI KUBORESHA MASLAHI YA WAFANYAKAZI WAO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wamiliki wa malori nchini wawajali madereva na wahudumu wa magari hayo ikiwa ni pamoja

Read More...

ZOEZI LA UOKOAJI HANANG, MAWAZIRI WAFIKA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista J. Mhagama, Waziri wa Ujenzi Innocent

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu