Trump aendelea kuikosoa China.

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ameishambulia China kwa jinsi ilivyoshughulikia mlipuko wa virusi vya a corona huku akisema janga hilo limekuwa na madhara makubwa kwa Marekani. Trump amewaambia waandishi habari mjini Washington kuwa ugonjwa wa COVID-19 usingesababisha athari kubwa iwapo Beijing ingefanikiwa kuudhibiti kikamilifu ulipozuka mwishoni mwa mwaka uliopita. Kiongozi huyo amesema Marekani imeathiriwa kwa kiwango kikubwa na janga la corona kuliko mashambulizi ya mabomu dhidi ya kambi ya kijeshi ya Pearl Harbor ya mwaka 1941 au tukio la kigaidi la Septemba 11. Hadi sasa zaidi ya watu 73,000 wamekufa nchini Marekani kutokana na ugonjwa wa COVID-19 na mkuu wa zamani wa taasisi ya kuzuia magonjwa nchini humo amebashiri idadi ya vifo inaweza kufikia 100,000 mwishoni mwa mwezi Mei.

Exit mobile version