Trump azidisha makali ya mvutano kuhusu mradi wa nyuklia.

Rais Donald Trump wa Marekani anazidisha makali ya mvutano kuhusu mradi wa nyuklia wa Korea Kaskazini, akisema huenda onyo lake la awali dhidi ya serikali ya mjini Pyongyang “halikuwa kali vya kutosha”.

Rais Trump ameyatoa matamshi hayo akiwa nyumbani kwake, Bedminster, katika jimbo la New-Jersey.

Trump amesema Korea Kaskazini inabidi iingiwe na taharuki kubwa hata kama inafikiria uwezakano wa kuihujumu Marekani au washirika wake, akitetea vitisho alivyotoa Jumanne iliyopita dhidi ya serikali ya Kim Jong-Un.

Hata hivyo rais Trump aliyeionya Pyongyang kuwa itakabiliwa na “moto na ghadhabu kubwa pamoja na nguvu ambazo ulimwengu haujawahi kushuhudia”. Ameitolea wito kwa mara nyengine China izidi kuishinikiza Korea Kaskazini, ingawa pia alisema Marekani iko tayari kwa mazungumzo.

Exit mobile version