Trump: Biashara inayowapendelea wengine haitakubalika.

In Kimataifa, Siasa

Rais Donald Trum wa Marekani amesema kuwa Marekani haitavumilia biashara yenye upendeleo, katika hotuba yake iliojaa malalamishi katika mkutano wa mataifa ya bara Asia na yale yaliopo katika bahari ya Pacific{Apec} mjini Vietnam.

Amesema kuwa Marekani imejiandaa kushirikiana na mataifa ya Apec iwapo kutakuwa na bishara yenye kutopendelea upande wowote.

Bwana Trump alisema kuwa biashara huru iliathiri kazi za mamilioni wa raia wa Marekani na sasa anataka usawa kutekelezwa.

Tayari ameitembelea China na Japan katika zaira yake ya mataifa matano ya bara Asia.Apec unaleta pamoja uchumi wa mataifa 21 kutoka eneo la Pacific ambao ni asilimia 60 ya uchumi wote duniani.

Tangu achukue mamlaka rais Trump ameiondoa Marekani katika muungano wa Trans-Pacific, ambao unahusisha mkataba mkubwa wa kibishara unaoshirikisha mataifa 12 ya Apec akidai kwamba utaathiri uchumi wa Marekani.

Katika hotuba yake siku ya Ijumaa rais Trump alilishutumu shirika la biashara duniani WTO ambalo hutengeza sheria za biashara duniani na kusema haliweza kufanya kazi zake vyema iwapo wanachama wake hawataheshimu sheria hizo.

Alilalamika kuhusu ukosefu wa usawa wa kibiashara akisema Marekani imeondoa vikwazo vya kibishara huku mataifa mengine yakikataa kufanya hivyo.

”Vitendo kama hivyo vinaathiri watu wengi katika taifa langu”, aliwaambia viongozi wa kibishara na wale wa kisiasa katka mkutano huo.

Lakini hakuyalaumu mataifa ya Apec na badala yake kulalamikia watawala wa awali wa Marekani kwa kutoingilia swala hilo na kurekebisha hali.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

Viwango vya maadili kwa viongoiz yaongezeka.

Imeelezwa kuwa viwango vya uzingatiwaji wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma nchini,vimeongezeka hadi kufikia asilimi 75.9 kwa

Read More...

Watu 193 wawekwa karantini kisa virusi vya Marburg.

Mganga Mkuu wa serikali Dkt Tumaini Nagu,amesema hakuna kisa kipya kilichoongezeka kuhusu vifo vilivyosababishwa na virusi vya Ugonjwa wa

Read More...

SERIKALI YAFANYA UWEKEZAJI MKUBWA KATIKA HUDUMA ZA HALI YA HEWA

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na uchukuzi,isemema kuwa katika kuhakikisha wanakuwa na Taarifa za uhakika za Hali ya hewa

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu