Trump: Chanjo ya virusi vya corona kupatikana kabla ya kumalizika 2020.

In Kimataifa

Rais Donald Trump wa Marekani amesema serikali yake itawekeza kwa makampuni yote makubwa yanayofanya jitihada za kutafuta chanjo ya virusi vya corona na kwamba imepunguza idadi ya makampuni hayo hadi kufikia 14, huku akitoa ahadi ya kuyapunguza zaidi. Katika mkutano wake uliofanyikia Ikulu ya Marekani, ambapo ulihudhuriwa na maafisa wengi wa Ikulu hiyo wakiwa wamevaa barakoa, lakini yeye akiwa hajavaa, Trump alionesha matumaiini kwamba kinga ya maradhi ya COVID-19 kabla ya kumalizika mwaka huu. Na kuongeza kusema serikali yake itashiriki vyema katika usambazaji wa chanjo hiyo pale tu, itakapopatikana. Hayo yanajiri wakati takwimu mpya zilizotolewa na chuo kikuu cha John Hopkins zinaonesha vifo vipya 1,680 ndani ya kipindi cha masaa 24 yaliopita.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu