Trump kukutana na viongozi wa Rwanda na DR Kongo Alhamisi

Rais wa Marekani Donald Trump atakutana na viongozi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Alhamisi hii ili kusaini makubaliano ya amani, Ikulu ya White House imesema.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio (katikati) katika hafla ya kusaini makubaliano ya amani na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Thérèse Kayikwamba Wagner (kulia) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe (kushoto) katika Wizara ya Mambo ya Nje mjini Washington, DC, tarehe 27 Juni 2025.
Exit mobile version