TUCTA yaiomba Serikali kuangalia kwa jicho lingine wafanyakazi zaidi ya elfu 9 waliobainika kugushi vyeti.

Shirikisho la vyama huru vya wafanyakazi Tanzania TUCTA-Mkoa wa Dar es salaam, limeiomba serikali kuangalia kwa jicho lingine wafanyakazi zaidi ya elfu 9 waliobainika kugushi vyeti ,badala ya kuwafukuza kazi kutokana na kuchangia nguvu zao katika kuleta maendeleo katika kipindi ambacho walikuwa kazini.
Ombi limetolewa na mwenyekiti TUCTA mkoa wa Dar es salaam George Faustine, wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani mkoani humo ambapo amesema kimsingi TUCTA, haiungi mkono suala la kugushi vyeti bali limeangalia utu na heshima ya mtu lakini pia shirikisho lina wajibu wa kumtetea mwanachama wake ,ili kuweka usawa baina yake na mwajiri.
Kwa upande wake mbunge wa urambo ambaye pia aliwahi kuwa rais wa kwanza TUCTA Magreth Sitta ambaye ni mgeni rasmi katika sherehe hizo ameiambia TUCTA kuwa ijenge utamaduni wa kuendesha wenyewe shughuli za maadhimisho hayo badala ya kutegemea viongozi kutoka serikalini kwani siku hiyo inatoa fursa kwao kujadili chanagamoto zinawakabili wafanyakazi
Exit mobile version