TUCTA yamtaka Rais Magufuli kutupia jicho sekta binafsi.

In Kitaifa
SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Mkoa wa Dar es Salaam, limemtaka Rais John Magufuli kutupia jicho sekta binafsi.
Pia, limesema linamuunga mkono Rais kwa kuwachukulia hatua wafanyakazi wa serikali zaidi ya 9,000 walioghushi vyeti, lakini linamuomba kuwatazama kwa jicho la huruma wafanyakazi hao, ambao wamesimamishwa kazi kuanzia leo, na kuwasamehe hasa wale waliobakiza miezi michache kustaafu.
Aidha, TUCTA imeomba serikali kuanza kuwachukulia hatua viongozi wa umma wakiwemo wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya, wanaowadhalilisha wafanyakazi kwa kuwatolea lugha za matusi na wengine kuwapiga, kwani vitendo hivyo pamoja na kuwavunjia heshima wafanyakazi hao pia vinawapunguzia morali wa kuwajibika.
Hayo yalibainishwa Dar es Salaam na Mwenyekiti wa shirikisho hilo mkoa wa Dar es Salaam, George Faustine, wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, iliyoadhimishwa jijini humo kimkoa.
Ametaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na kutozwa kodi kubwa katika mishahara ya wafanyakazi, huku wafanyakazi hao wakiendelea kununua bidhaa ambazo pia zinatoza kodi na hivyo kuongeza mzigo wa maisha kuwa magumu kwa wafanyakazi hao.
Kwa upande wake, Mwenyekiti mstaafu wa TUCTA na Mbunge wa Urambo, Margaret Sitta ,amewataka wafanyakazi kuhakikisha wanajiunga na vyama vya wafanyakazi ili kuongeza umoja katika kudai haki zao, lakini pia kujiwekea mazingira mazuri ya kufanya kazi.
Maadhimisho hayo yalianza kwa maandamano kutoka taasisi, Kampuni na mashirika mbalimbali ,ikiwemo kutangaza bidhaa zao mbele ya wageni waliohudhuria sherehe hizo.

Join Our Newsletter!

Get updates, news etc from us. Its simple just put in your email address.

You may also read!

WANAFUNZI 500 WAPEWA MBINU WASILOWEE KWENYE MADAWA YA KULEVYA.

Na Tonie kaisoe ,Arusha Wanafunzi zaidi ya 500 wa shule ya Sekondari Arusha Jiji na Wilaya ya Arumeru wamepewa mbinu

Read More...

MR. IBU AFARIKI DUNIA

Mchekeshaji maarufu wa Nollywood nchini Nigeria, John Okafor, almaarufu Mr. Ibu amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Read More...

POLISI, LATRA WAPIGA FAINI MABASI YALIYO ZIDISHA NAULI ARUSHA.

Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Arusha kwa kushirikaiana na Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA)

Read More...

Leave a reply:

Your email address will not be published.

Mobile Sliding Menu