Linapokuja swala la mafanikio zipo sifa na mambo mengi ambayo, yanakuwa yanatajwa katika kumfikisha mtu ili aweze kufanikiwa.
Hata hivyo pamoja na sifa hizo ipo sifa moja muhimu sana, ambayo kwa mtafuta mafanikio kama unayo ni lazima utafanikiwa.
Sifa hii muhimu ya kimafanikio sio nyingine bali ni sifa ya uvumilivu.
Unaweza ukawa unajituma kweli, una nidhamu binafsi na unafanya juhudi za kuwekeza kila wakati, lakini ukikosa uvumilivu huwezi kufanikiwa.
Uvumilivu ni kitu cha muhimu sana kama umeamua kuishi maisha ya ndoto zako.
